Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 6:18:19
  • More information

Informações:

Synopsis

Paula na Philip ni wahariri wa Radio D wanaochunguza visa vya ajabu. Andamana na wachunguzi hawa shupavu kote Ujerumani na uimarishe Kijerumani chako na uwezo wa kusikiza na kuelewa pia.

Episodes

  • Tukio 06 – Mfalme Ludwig alifariki vipi?

    24/08/2009 Duration: 13min

    Katika Kasri la Neuschwanstein, Paula na Philipp wanakutana na mgeni wasiyemwelewa ambaye amevaa joho la Mfalme Ludwig. Wanafanya uchunguzi kuhusu utata unaogubika kifo cha Ludwig. Mwanamume aliyejitanda mabegani mwake joho la Mfalme Ludwig anajaribu kuwasadikisha Paula na Philipp kwamba yeye ni marehemu mfalme. Je Ludwig alifariki vipi? Waandishi hao wawili wa habari wanatayarisha mchezo wa redio kuwaeleza wasikiliza wao kuhusu nadharia kadha wa kadha za kifo cha Mfalme Ludwig katika Ziwa la Starnberg. Hakuna anayejua kwa uhakika ikiwa aliuliwa au alijiua. Mkutano na mtu huyo asiyeeleweka ni fursa nzuri ya kusikia tofauti za kawaida zilizopo kati ya kuzungumza na rafiki au mgeni. Sikiliza kiwakilisha rasmi "Sie" na kiwakilishi kisicho rasmi "du." Kitenzi-jina cha kitenzi "kuwa" – "sein" ni.

  • Tukio 05 – Mfalme Ludwig bado yu hai!

    24/08/2009 Duration: 14min

    Paula na Ayhan wanamkaribisha mfanyikazi mwenzao mpya katika Radio D. Tayari wana jukumu muhimu la kutekeleza. Marehemu Mfalme Ludwig wa Bavaria anasemekana angali hai na kundi hilo linataka kuchunguza kadhia hiyo. Philipp anakutana na wafanyikazi wenzake wapya Paula na Ayhan, na pia Josefine ambaye anasimamia taratibu za afisini. Hapana muda wa kupoteza maana Philipp na Ayhan tayari wanajua habari yao ya kwanza. Kuna tetesi kwamba mfalme maarufu Ludwig wa Pili wa Bavaria angali hai, ingawa alisemekana alifariki kwa njia isiyoeleweka mwaka 1886. Waandishi habari hao wawili wanaelekea katika Kasri la Neuschwanstein kuchunguza na kujifahamisha. Mambo yasiyoeleweka yanazua maswali mengi. Katika tukio hili unaweza kufahamu zaidi maneno ya kuulizia maswali na majibu.

  • Tukio 04 – Kumsubiri mfanyikazi mwenza mpya

    24/08/2009 Duration: 13min

    Wafanyikazi wa kitengo cha uhariri cha Radio D wanamsubiri Philipp. Paula na Ayhan, watakaofanya kazi na Philipp, wanajifurahisha. Philipp haonekani na simu hazifanyi kazi. Philipp amechelewa sana kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. Anajaribu kumpigia simu Paula ili amjulishe, lakini hampati. Philipp anatatizika zaidi kwa sababu ya simu anayopokea kutoka kwa mama yake. Philipp anaomba radhi kwa kuchelewa kwake. Katika tukio hili, utasikia misemo tofauti ya kuomba radhi na kutoa udhuru.

  • Tukio 03 – Ziara ya Berlin

    24/08/2009 Duration: 14min

    Philipp anaelekea Berlin. Hali ya hewa inamtatiza sana. Akiwa safarini, Philipp anajuana na watu kadhaa. Philipp anasafiri kwa gari kwenda Munich anakotumai kupanda ndege ya kuelekea Berlin. Safari yake inachukua muda mrefu zaidi kutoka na mvua kubwa. Katika tukio hili, wafanyi kazi wa Radio D, Philipp na mama yake wanajitambulisha kwa ufasaha zaidi. Utasikia wakijitambulisha kwa njia rasmi na njia isiyo rasmi.

  • Tukio 01 – Ziara mashambani (Vijijini)

    24/08/2009 Duration: 15min

    Philipp, ambaye ni kijana, anasafiri kwa gari kwenda mashambani kumtembelea mama yake Hanne. Anatumai kupunga hewa lakini punde anagundua kuwa mashambani pia kuna vitimbi vyake. "Mandhari asilia, raha iliyoje!" Philipp anasema punde anapowasili nyumbani kwa mama yake mashambani, ambako anataka kujipumzisha. Huko kuna zaidi ya paka na ng'ombe. Philipp anapokunywa kikombe chake cha kahawa kwenye bustani, hapati amani aliyoitaraji kwani wadudu wanamsumbua si haba—kisha mambo yanamharibikia Philipp. Hata kama huna msamiati wa kutosha bado, unaweza kufahamu tukio hili. Sauti zinasosikika chini kwa chini zinaashiria mahali Philipp alipo. Katika tukio hili, utajifunza maamkizi na kauli za kuagana.

  • Tukio 02 – Simu kutoka Radio D

    24/08/2009 Duration: 13min

    Philipp hajapata amani yoyote wala utulivu. Baada ya kusumbuliwa na wadudu, inambidi kukabiliana na majirani wasioisha kelele. Anapopigiwa simu asiyoitarajia kutoka Berlin, anaondoka haraka. Usumbufu aliopata kutokana na wadudu si lolote si chochote! Maji yanamfika shingoni Philipp anapokabiliana na kelele za msumeno wa umeme pamoja na mpiga tarumbeta limbukeni. Paula kutoka Radio D mjini Berlin anapompigia simu, Philipp anapata kisingizio cha kukatiza ziara yake. Mama yake Philipp anasikitika sana pale Philipp anapomuaga na kuelekea mji mkuu wa Ujerumani. Hata kama huna msamiati wa kutosha bado, unaweza kufahamu tukio hili. Maneno ya kimataifa na kiimbo vitakuwezesha kufahamu mtiririko wa tukio na pia kufanya mazoezi ya ufahamu kwa kusikiliza.

page 2 from 2