Habari Za Un

WFP: Bila msaada wa kibinadamu Wasudan watakufa kwa njaa

Informações:

Synopsis

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa. Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika ukurasa wake wa X leo Oktoba 28 na kufafanua zaidi kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili nchini humo anatatizika kupata mlo kila siku.WFP inaeleza kuwa njaa imethibitishwa Kaskazini mwa Darfur na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana.Kabla ya taarifa hii ya leo ya WFP, jana kupitia pia ukurasa wa mtandao wa X, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Cindy McCain ambaye hivi karibuni alikuwa Sudan mojawapo ya maeneo yenye njaa zaidi duniani, ambapo watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali ameandika kwamba WFP iko Sudan inatoa msaada wa kuokoa maisha lakini wanahitaji kwa haraka mambo matatu ambayo ni kuwafikia watu ili kuwasaidia, misaada kuweza kupita katika kila kivuko na usaidizi zaidi wa kimataifa kwa Wasudani wa