Habari Za Un
04 NOVEMBA 2024
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:49
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan unaosababisha janga la njaa, na mradi wa maji Galmudug Somalia kwa ajili ya maji safi na salama pamoja na mifugo. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.Makala inakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Kapteni Fadhillah Nayopa, Afisa habari wa kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania, TANZBATT-11 katika ujumbe wa Umoja wa Matai