Synopsis
Andreas ana shughuli nyingi za kufanya. Inambidi kushughulikia wageni hotelini, kuwatafutia wazazi wake chumba na pia kumhoji Charlemagne. Ziada ya hayo, wazazi wake wanamchunguza ex ni nani na wapi alikutana na binti yao. Mambo muhimu ya sarufi: Vitenzi vya utaratibu, wakati timilifu, uhusika usioungwa moja kwa moja.
Episodes
-
Somo 26 – Safari ya kwenda Loreley inapendeza ajabu
18/03/2009 Duration: 15minEx mara ametoweka... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
-
Somo 25 – Unaweza kunipatia taulo za mkono?
18/03/2009 Duration: 14minAndreas, Dr. Thürmann na Frau Berger wanaandaa safari ya meli... Muhtasari wa sarufi: Vitendo vyenye uhusika wa ‚dative‘ na ‚accusative‘
-
Somo 24 – Nimesahau
18/03/2009 Duration: 15minKumtembelea mgonjwa Dr. Thürmann. Muhtasari wa sarufi:Wakati timilifu wa vitendo visivyotenganishwa
-
Somo 23 – Kumetokea nini?
18/03/2009 Duration: 15minAndreas anapokea simu kutoka mtu anayemjua... Muhtasari wa sarufi: Wakati timilifu (perfect tense) wa vitendo vinavyotenganishwa
-
Somo 22 – Jumatano saa moja ya asubuhi
17/03/2009 Duration: 15minMatatizo Hotel Europa: Bomba la mvua (shower) limeharibika... Muhtasari wa sarufi: Kiulizio cha wakati
-
Somo 21 – Posta iko wapi (Nitafika vipi posta)?
17/03/2009 Duration: 14minMtafaruku katika mapokezi ya hoteli... Muhtasari wa sarufi: Kijineno denn
-
Somo 20 – Nimeandikisha chumba (hotelini)
17/03/2009 Duration: 15minSiku ya kukosa bahati Herr Müller... Muhtasari wa sarufi: Uhusika usioungwa moja kwa moja (dative case III)
-
Somo 19 – Mtu humsemesha vipi Kaizari?
17/03/2009 Duration: 16minMahojiano na Karl Mkuu ... Muhtasari wa sarufi: Uhusika usioungwa moja kwa moja (dative case II)
-
Somo 18 – Yeye kaniambia hayo
17/03/2009 Duration: 14minMazungumzo kuhusu siri za Aachen... Muhtasari wa sarufi: Uhusika usioungwa moja kwa moja (dative case I)
-
Somo 17 – Asili ya jina Aachen inatoka wapi
17/03/2009 Duration: 13minRipoti ya Andreas: maandalizi ya mwanzo ya kikazi... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
-
Somo 16 – Kuna (mtu) aliyesikia hayo
17/03/2009 Duration: 17minAndreas anatoa siri yake... Muhtasari wa sarufi: Wakati timilifu (perfect tense) kwa kitendo haben
-
Somo 15 – Jambazi liitwalo Mack the Knife (Meki Majisu)
17/03/2009 Duration: 16minAndreas na Ex kabla ya kwenda kutazama mchezo wa kuigiza... Muhtasari wa sarufi: Uhusika usioungwa moja kwa moja (dative case) kwa majina ya kiume (masculine nouns)
-
Somo 14 – Insemekana (mchezo huo) unavutia sana
17/03/2009 Duration: 16minMvutano kuhusu mchezo upi wa kuingiza unafaa... Muhtasari wa sarufi: Kielezi cha pahali wo. Kitendo cha utaratibu sollen
-
Somo 13 – Unayo pia sketi hiyo ya rangi nyeusi?
17/03/2009 Duration: 14minMama yake Andreas yuko katika duka kubwa... Muhtasari wa sarufi: Kuunganisha majina (nomino)
-
Somo 12 – Masomo yanaendelea vizuri sana
17/03/2009 Duration: 12minBaba yake Andreas ana matatizo.. Muhtasari wa sarufi: Uhusika usioungwa moja kwa moja (dativ case) wa kidhihirishi kikamilifu (definite article) na viwakilishi vya binafsi.
-
Somo 11 – Pengine katika jumba la michezo ya kuigiza?
17/03/2009 Duration: 14minMijadala migumu katika familia ya Andreas... Muhtasari wa sarufi: Kuuliza kwa kutumia neno wohin
-
Somo 10 – Siku zote unataka kujua kila kitu
17/03/2009 Duration: 13minMama yake Andreas anataka kujua mengi... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu wollen
-
Somo 09 – Mimi ningependa ndizi!
17/03/2009 Duration: 14minFriji la Andreas ni tupu tena... Muhtasari wa sarufi: Majina bila ya vidhihirishi
-
Somo 08 – Hilo usilifanye!
17/03/2009 Duration: 14minSimu inalia: Wazazi wa Andreas wanakuja... Muhtasari wa sarufi: Vitendo vya utaratibu sollen na müssen
-
Somo 07 – Ndege yangu inaondoka saa tatu
17/03/2009 Duration: 15minKwenye mapokezi ya hoteli: Mgeni mmoja ana haraka... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu dürfen