Habari Za Un
UNICEF nchini Ethiopia yarejesha matumaini kwa manusura wa ukatili wa kingono
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:51
- More information
Informações:
Synopsis
Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15. Sauti hiyo ya Nasteyo Sahane Layle, Meneja wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia dhidi ya akina mama, watoto na wanawake hapa Gode, jimboni Somali mashariki mwa Ethiopia akisema kuwa kazi kubwa tunayoifanya ni visa vinavyohusu ukatili wa kingono.Ni katika video ya UNICEF iliyochapishwa kuonesha kiza kinachokumba watoto wa kike hususan leo ambayo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.Hapa Gode, UNICEF imeanzisha kituo hicho cha kutoa huduma zote na sasa kimekuwa ni kama eneo salama kwa manusura wa ukatili wa kingono.Anaonekana mmoja wa wasaka huduma kituoni hapa akifika tayari kupatiwa huduma, su