Habari Za Un
Patricia Kombo COP29: Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:51
- More information
Informações:
Synopsis
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana. Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema“Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”Na