Siha Njema
Magonjwa ya Autoimune yana uwezo kukusababishia magonjwa mengine zaidi
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:10:23
- More information
Informações:
Synopsis
Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo. Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune. Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au Autoimmune,watalaam wanasikitika kuhusu ufahamu mdogo kuhusu magonjwa haya. Wagonjwa wengi huwa na dalili za kukanganya na ubainishaji wa magonjwa haya unaweza kuchukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa cha pesa. Na kwa kuwa vyanzo vya magonjwa haya huwa haviko wazi matibabu yake huwa yenye mtihani mkubwa.Watalaam wengi hujaribu kutibu dalili bila kushughulikia chanzo cha ugonjwa wenyewe. Katika makala haya tumezungumza na Elwyn Chebet ambaye ni shujaa na mwanaharakati wa ugonjwa wa Lupus ambao huathiri viungo kadhaa mwilini na hata ngozi. Katika simulizi yake ,anaeleza kuwa kutokana na kinga dhaifu magonjwa tegemezi ka