Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Sanaa ya Uchongaji Vinyago nchini Tanzania
16/11/2024 Duration: 20minSteven Mumbi amezungumza na Lyala Sebastian Mchongaji wa Sanaa za Vinyago.
-
Sanaa ya uchoraji wa vinyago na fursa wa biashara inazoleta
09/11/2024 Duration: 20minWabunifu wa Sanaa ya Uchongaji Vinyago wamewekeza katika kung'amua fursa ya biashara kwa Mataifa ya Afrika Mashariki ili kujikwamua na vipato Duni, Steven Mumbi amezungumza na Mintanga Ramadhani Msanii wa Sanaa za Uchongaji Vinyago kutoka nchini Tanzania.
-
Muziki wa HIP HOP nchini Tanzania
26/10/2024 Duration: 20minMuziki wa HIP HOP nchini Tanzania umefifia kutokana na ugumu wa kufanya Muziki huo,Msanii PMawenge anasimulia hatua za kuchukua kuurejesha sokoni katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Tanzania: Sanaa ya ushairi na msanii Michael James maarufu Michael
28/09/2024 Duration: 20minSanaa ya ushairi inawavutia zaidi watu wanaotamani kujua utamu na upekee wa lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatambua na kuwapa fursa vijana waliosomea fani ya sanaa, kubobea katika kughani Mashairi. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii Michael James maarufu Michael.
-
-
Tanzania: Tunazungumza na kundi la wasani la viongozi generation
14/09/2024 Duration: 20minMwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na kundi la wasani la viongozi generation.
-
Tanzania: Muziki wa kizazi kipya na Hussein Mussa Shundi Maarufu Rucky
07/09/2024 Duration: 20minMuziki wa kizazi kipya umewawezesha vijana nchini Tanzania kujikwamua kimaisha kwa kujipatia kipato kupitia Sanaa hiyo,Katika Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Hussein Mussa Shundi Maarufu Rucky.
-
Mwanza: Msanii wa Bongo Fleva, Baraka the Prince ndiye mgeni wetu wiki hii
31/08/2024 Duration: 20minMsanii wa Bongo Fleva, Baraka the Prince anauona muziki ni maisha, jambo linalomfanya afikirie zaidi namna mashabiki wake wataishi na kazi zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.
-
Tanzania: Wiki hii tunaliangazia kundi la Muziki la The Mafiki
24/08/2024 Duration: 20minThe Mafiki ni kundi la Muziki lililovuma kwa vionjo vya Muziki wa sasa, sasa wamekuja upya mara baada ya kusambaratika, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii wa kundi hilo.
-
Muziki wa Taarab nchini Tanzania naye Jike la Chui
17/08/2024 Duration: 20minMapinduzi ya Muziki wa Taarab yanajidhihirisha katika tenzi za wasanii wa Muziki huu kutoka tungo za Majigambo na sasa tungo za kuburudisha, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Jike la Chui.
-
Zumbukuku nyimbo za taarab zinazokumbukwa hata sasa
03/08/2024 Duration: 20minZumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
-
Mwanamuziki Ogisha Matale atoa wito wa amani mashariki mwa DRC
27/07/2024 Duration: 20minMakala ya nyumba ya sanaa wiki hii imepiga kambi mjini Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako mwanzoni mwa mwezi mei mwandishi wetu Ruben Lukumbuka alikutana na msanii Ogisha Matale ambapo katika shughuli zake zake amekuwa akijaribu kuhimiza amani nchini, hususan eneo lake lenye kushuhudia mapigano ya mara kwa mara.
-
Mwanamziki Nyota Tiger mwalikwa wa makala Nyumba ya sanaa
20/07/2024 Duration: 20minNyota Tiger ni mzaliwa wa jijini Mwanza nchini Tanzania alilazimika kusafiri mpaka maeneo ya kusini mwa Afrika kukwepa adha za wazazi kumnyima fursa ya kufanya muziki. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Mchango wa sanaa ya muziki wa asili katika usuluhishi wa mizozo DRC
13/07/2024 Duration: 20minKatika makala ya nyumba ya sanaa wiki hii mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mashariki mwa DRC ambako alikutana na Olivier wabahavu, msanii maarufu sana kufuatia nyimbo zake anazoimba katika lugha ya kihavu na kishi huko Kivu kusini na kaskazini, amezungumzia mchango wa sanaa ya muziki wa kiasili katika usuluhishi wa migogoro ya kivita mashariki mwa DR Congo.
-
Tanzania: Muziki wa Singeli na Man Fongo
06/07/2024 Duration: 20minMuziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaokua kwa kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika,Wasanii wa Muziki huo wanapambana kuukuza Kimataifa, Man Fongo ni Miongoni mwa Wasanii Pendwa wa Muziki huo,Ungana na Steven Mumbi anazungumza na Msanii huyo.
-
Tanzania: Muziki wa asili na Jilema Ng'wana Shija
29/06/2024 Duration: 20minKatika Makala ya Wiki hii, Steven Mumbi amezungumza naye Jilema Ng'wana Shija msani wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania.
-
Nyumba ya sanaa na msanii Tourna Boy kuhusu muziki wa kizazi kipya
22/06/2024 Duration: 20minKaribu katika makala ya Nyumba ya sanaa nami Steven Mumbi, hii leo Msanii Tourna Boy wa kizazi kipya kutoka mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akielezea kuhusu juhudi za vijana wasanii kuchangia katika juhudi za kurejesha amani ya mashariki mwa nchi hiyo, katika mazungumzo na mwenzangu Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo la Goma mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu 2024
-
Muziki wa Singeli na Torino Abdul Sykes kutoka Mbagala Tanzania
08/06/2024 Duration: 20minKwenye Makala ya wiki hii Stephen Mumbi anazungumza na msani Abdul Sykes kutoka Mbagala Tanzania.
-
Wasanii wa mashariki ya DRC wachangia juhudi za upatikanaji wa amani
01/06/2024 Duration: 20minMakala ya Nyumba ya sanaa wiki hii inamuangazia msanii wa muziki wa regae Mack El Sambo ambaye kwa zaidi ya miaka ishirini amekuwa akihimiza amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, hususan kwenye mji wa Goma katika mkowa wa Kivu Kaskazini. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mji wa Goma na kukutana na mwanamziki huyu..
-
DRC: Ubunifu wa viatu vya ngozi mjini Goma na Christian Bazika
25/05/2024 Duration: 20minKatika Nyumba ya sanaa wiki hii Steaven Mumbi akishirikiana na Ruben Lukumbuka ambaye wiki iliyopita alitembelea mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako alikutana na mbunifu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ubunifu wa kutengeneza viatu bwana Christian Bazika anayetengeneza bidhaa za ngozi mashariki mwa nchi hiyo.