Synopsis
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
Episodes
-
Mzozo kati ya Rwanda na Uganda kuhusu mpaka wa Katuna
06/03/2019 Duration: 11minNchi za Rwanda na Uganda zinashuhudia mvutano wa kidiplomasia. Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwaficha maadui wa serikali yake, suala ambalo Uganda inakanusha vikali.
-
Mustakabali wa DRC baada ya matokeo ya uchaguzi
31/01/2019 Duration: 11minBaada ya tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kumtangaza mshindi wa kiti cha uraisi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi,tunaangazia nini matarajio ya raia sasa,nini mustakabali wa DRC wakati huu upinzani wa lamuka ukipinga matokeo hayo kwa kudai udanganyifu ulifanyika.
-
Mzozo wa kisiasa nchini Venezuela
30/01/2019 Duration: 11minVenezuela imejikuta katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi, kiongozi wa upinzani Juan Guaido amejiapisha kuwa rais, huku kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro akitishia kumchukulia hatua kali. Tunajadili hili kwa kina.
-
Wananchi wa DRC bado wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu
09/01/2019 Duration: 17minMamilioni ya raia wa DRC, pamoja na dunia, inasubiri Tume ya Uchaguzi kumtangaza mshindi wa Uchaguzi wa urais, baada ya wananchi kupiga kura Desemba 30 2018. Nani atashinda Uchaguzi huu na ni kwanini matokeo yamechelewa ? Tunachambua suala hili kwa kina.