Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Kwa nini ni muhimu kuwafikiria akina mama na watoto kwenye kampeni ya magonjwa yaliyosahaulika
02/12/2025 Duration: 09minRipoti nyingi huonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ni akina mama au watoto Hii ni kutokana na wao kutangamana moja kwa moja na mazingira ambayo huwa makazi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa mbali mbali. Vimelea hao hukaa mchangani,kwenye maji au hupatikana kwenye kinyesi .
-
Mabadiliko ya tabia nchi yanayovyochochea magonjwa ya milipuko
01/12/2025 Duration: 10minTafiti zimeonesha kuwa magonjwa mengi ya milipuko haswa barani Afrika yanachochewa na mabadiliko ya tabia nchi Mafuriko ,ukame au kupanda joto yanaweza kusababisha kusambaa kwa haraka kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa au kuzaana kwa haraka.
-
Mzigo wa ugonjwa wa Kisukari nchini Sudan Kusini unavyowawaliza wengi
19/11/2025 Duration: 09minSudan Kusini kando na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kisukari ,upatikanaji wa matibabu bado ni changamoto kubwa Watalaam nchini humo wanahoji mabadiliko ya mtindo wa maisha kama chanzo cha ongezeko la visa hivi.
-
Takwimu sahihi za mapema na maabara wezeshi kupambana na magonjwa ya milipuko
12/11/2025 Duration: 09minWHO inashauri ukanda wa Afrika kuwekeza zaidi katika takwimu zilizo sahihi katika mikakati ya kupambana na magonjwa ya milipuko