Synopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodes
-
Sudan yampata Waziri Mkuu, vita vikiendelea kupamba moto
04/06/2025 Duration: 10minUongozi wa kijeshi nchini Sudan mwishoni mwa mwezi Mei, ulimteua mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe Kamil Idris, kuwa Waziri Mkuu mpya wakati huu vita vikiendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. Tangu kuanza kwa vita Aprili 2023, watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha, huku wengine Milioni 15 wakikimbia makaazi yao, wakiwemo zaidi ya Milioni nne ambao wamekimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Nini hatima ya Sudan ?
-
DR Congo: Kabila aondolewa kinga ya kutoshtakiwa, aripotiwa kufikia Goma
28/05/2025 Duration: 10minMaseneta nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemwondolea kinga ya kutoshtakiwa rais wa zamani Joseph Kabila , ambaye ripoti zinasema alirejea Goma usiku wa Mei 25.Kiongozi huyo wa zamani, ameishtumu serikali ya rais Felix Tshisekedi na kuuita ya Kidikteta. Hata hivyo, serikali ambayo inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kushirikiana na waasi wa M23.
-
Wanaharakati kutoka Kenya wafukuzwa nchini Tanzania
21/05/2025 Duration: 10minWanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, akiwemo Martha Karua na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, walifukuzwa nchini Tanzania, Mei 19, walikokuwa wamekwenda kama mashuhuda wa kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa nchi yake haitaruhusu wanaharakati kutoka nje, kuvunja amani ya nchi yake. Tunachambua kilichotokea nchini Tanzania.
-
Uganda: Serikali yawasilisha mswada bungeni, kutaka raia kushtakiwa kwenye Mahakama za kijeshi
14/05/2025 Duration: 10minMswada tata, utakaoruhusu raia wa kawaida kushatakiwa kwenye Mahakama za kijeshi, umewasilishwa bungeni nchini Uganda, Mei 13, 2025. Upinzani unasema, lengo la mswada huo ni kuwalenga wanaopinga kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2026. Kwanini serikali ya Uganda inataka raia wa kawaida washtakiwe kwenye Mahakama za kijeshi ?