Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:59:24
  • More information

Informações:

Synopsis

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Episodes

  • Vitabu: Kampeni ya kuwafikia watoto milioni moja kuhusu uhifadhi

    23/06/2025 Duration: 10min

    Watoto wana jukumu muhimu katika uhifadhi wa mazingira na wanyamapori kwa kushiriki kikamilifu katika mipango kama vile kupanda miti, udhibiti wa taka, na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mazingira na wanyamapori. Kuwashirikisha watoto katika shughuli hizi kunakuza hisia ya uwakili, kuwaunganisha na mazingira wanayoishi, na kukuza mazoea endelevu kwa siku zijazo.

  • Mgogoro wa Bahari: Afrika yataka kushirikishwa kikamilifu katika ulinzi wa bahari

    19/06/2025 Duration: 10min

    Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kutekeleza lengo nambari 14 la Maendeleo Endelevu, ulifanyika kule Nice, Ufaransa, kujadili mbinu mwafaka za kuhifadhi na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake, washikadau wakiunda uhusiano mpya kati ya wanadamu na mazingira ya baharini. Mkutano wa kilele ulikamilika Ijumaa tarehe 13 Juni, 2025 wakati huu mataifa yakitarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili sheria za uchimbaji madini kwenye kina kirefu cha maji baharini.

  • Uhifadhi wa baharini: Hospitali ya kasa Pwani ya Kenya yatoa ahueni kwa viumbe hao

    09/06/2025 Duration: 10min

    Mataifa yametakiwa kuchukua misimamo mikali kuhusu uvuvi wa kupindukia, uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini.

  • Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Mazingira, taka za plastiki suala kuu

    02/06/2025 Duration: 10min

    Uchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.

page 2 from 2