Synopsis
Mission Europe ni somo la lugha lenye sehemu tatu: Mission Berlin, Misja Kraków na Mission Paris. Jitose kwenye bahari ya lugha ujifunze, Kijerumani.
Episodes
-
Mission Berlin 06 – Mripuko wa Zamani
20/03/2009 Duration: 05minAnna anakutana na mtu mwingine anayeonekana kama anayefahamiana naye. Mara hii ni mwanamke anayesema walikuwa marafiki mwaka 1961. Anna anazidi kutatizika kwa habari kwamba kuna mwanamke anamwandama. Watu ambao Anna hawafahamu wanajitokeza kila pembe. Mara hii ni mwanamke. Anasema yeye na Anna waliishi chumba kimoja mwaka 1961 na kwamba anataka kumsaidia Anna kutekeleza jukumu lake la hatari. Heidrun Drei anamtahadharisha Anna kujichunga na mwanamke aliyevaa mavazi mekundu ambaye anamwandama. Lakini Heidrun Drei hayo yote ameyajulia wapi?
-
Mission Berlin 05 – Tumewahi kukutana?
20/03/2009 Duration: 05minAnna anakipeleka kikasha chake cha muziki kwa mtengeza-saa ili kitengenezwe. Paul Winkler anaikubali kazi hiyo na kumwambia Anna kuwa anamjua tangu kitambo. Inawezekana vipi? Anna ndio kwanza amewasili. Kikasha cha muziki kinapofunguliwa, kinaonekana kimeharibika zaidi. Paul Winkler anapata kipande cha karatasi kilichoandikwa tarakimu hizi 19610813. Zina maana gani? Na je Paul Winkler anazungumzia nini? Anna anamuomba amtengeneze saa, naye anasema wanajuana tangu kitambo. Katika hali hii ya butwaa, Anna anajitahidi kuokoa muda na ana dakika 90. Amefuata muziki kama maandishi yalivyopendekeza lakini nini maana ya "mgawanyiko ndio suluhisho"?
-
Mission Berlin 04 – Dalili za Hatari
20/03/2009 Duration: 05minAnna anawasili mahali aliponuia katika Kantstraß3 lakini pamefungwa. Anaambiwa mwenyewe yumo mkahawani. Inaonekana kana kwamba wanajuana. Anna anahitaji dakika 100. Je ana muda wa kutosha? Anna anachanganyikwa kabisa anapokuta duka limefungwa. Leo Winkler amefariki. Mpiga kinanda anamweleza Anna kuwa mmiliki mpya wa duka ni Paul, mwanawe Leo Winkler. Anakunywa kinywaji chake cha kila siku cha kakao moto kwenye mkahawa wa karibu. Anakwenda mkahawani na kuagiza kahawa… Kaffee…na kuna bwana mwenye kidani cha fedha chenye umbo la fidla anayetabasamu. Ogur anaingia mkahawani na kumwambia Anna kwamba jukumu lake hilo ni hatari … gefährlich … kama ilivyo RATAVA. Anna anataka kudadisi na anamfuata bwana huyo mzee aliye na fidla. Lakini kadhia hii ina nini?
-
Mission Berlin 03 – Kuelekea Kantstraße
20/03/2009 Duration: 05minAnna anaelekea Kantstraße lakini anachelewa kwa kuwa inambidi kuulizia njia. Anapoteza muda zaidi wakati watu wenye pikipiki wanapofika na kumfyatulia risasi. Kazi ya Anna inakabiliwa na vikwazo. Anapowataka watoto waliyovaa vitau vyenye magurudumu kumwelekeza njia, wenye pikipiki wanampiga risasi. Mchezo unapoanzishwa tena, hatimaye Anna anawasili Kantstraße. Lakini je atapata anachotafuta?
-
Mission Berlin 02 – Mambo Bado
20/03/2009 Duration: 05minAnna anaanza kujibu maswali ya Ogur lakini anakatizwa na sauti ya pikipiki pamoja na milio ya risasi. Anakimbilia kwenye makumbusho anakopata anwani juu ya kasha lake la muziki. Je anwani hii itamfaa? Anna anajificha kwenye jumba la makumbusho. Anajificha ndani ya choo cha wanaume kwa kuwa ana wasiwasi huenda polisi au wenye pikipiki walio na silaha wangali wanamwandama. Hapo anagundua anwani ya Leo Winkler katika barabara ya Kantstraße iliyoandikwa kwenye kasha lake la muziki. Je huyo bwana yu hai na je anaweza kumsaidia Anna?
-
Mission Berlin 01 – Kiroja
20/03/2009 Duration: 05minJukumu la Anna ni kuinusuru Ujerumani isifikwe na janga. Ni lazima aihifadhi siri, atengue kitendawili, na kuwachunguza wanaume wenye pikipiki. Anahitaji dakika 130. Dalili ya kwanza i wapi? Anna anaamka katika chumba namba 14 … Zimmer vierzehn, kwenye mkahawa mmoja nchini Ujerumani. Wakati huo huo Kamanda wa Polisi anaelekea chumbani kwa Anna. Kamanda Ogur anajitambulisha na anagusia mauaji ya mgeni kwenye chumba nambari 40. Zimmer vierzig. Kwenye kioo cha bafu anatambua maandishi "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik". Anna anaanza kujibu maswali ya kamanda. Lakini maandishi hayo yana maana gani?