Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
DRC: Ubunifu wa viatu vya ngozi mjini Goma na Christian Bazika
25/05/2024 Duration: 20minKatika Nyumba ya sanaa wiki hii Steaven Mumbi akishirikiana na Ruben Lukumbuka ambaye wiki iliyopita alitembelea mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako alikutana na mbunifu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ubunifu wa kutengeneza viatu bwana Christian Bazika anayetengeneza bidhaa za ngozi mashariki mwa nchi hiyo.
-
-
Tanzania: Sanaa ya uigizaji, tunamuangazia Asha Jumbe maarufu White Maria
11/05/2024 Duration: 20minAsha Jumbe maarufu White Maria ni Muigizaji aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa Miaka nane tu, sasa ni mtu Mzima aja kivingine kufanya sanaa ya Fimalu za kiswahili,Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia safari yake ya Uigizaji.
-
Wiki hii makala haya yanamuangazia Steven Ibrahim maarufu Eddy Music
04/05/2024 Duration: 20minSanaa ya Muziki imenihitaji kuliko nilivyo ihitaji, ni kauli yake Steven Ibrahim maarufu Eddy Music alipozungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.