Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Informações:

Synopsis

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episodes

  • Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yamerejelewa jijini Nairobi, Kenya

    11/05/2024 Duration: 19min

    Katika makala ya wiki hii baadhi ya matukio ya ulimwengu tutakayoangazia ni mazungumzo ya kutafuta amani nchini Sudan Kusini ambayo yalianza Alhamisi jijini Nairobi, lakini pia madaktari nchini Kenya kusitisha mgomo wa siku 56, vilevile kule DRC, shirika la OCHA kusema kuongezeka kwa mapigano huko Kivu Kaskazini kumesababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao. Nchi ya Chad, ina rais mpya ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno, kadhalika tutaangazia hali kule Gaza na nchini Ukraine.

  • Athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki haswa nchini Kenya

    04/05/2024 Duration: 20min

    Wiki hii baadhi ya mambo tunayoangazia ni athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki, pia mgogoro kule Sudan, lakini pia kauli ya Ufaransa kwa Rwanda kuacha kuunga mkono kundi la M23 kule DRC. Kadhalika tutaangazia uhuru wa vyombo vya habari kuminywa nchini Burkina Faso lakini pia kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

  • Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika ,mafuriko yaripotiwa Kenya

    27/04/2024 Duration: 19min

    Makala haya yanaangazia yaliyojiri nchini Kenya na Tanzania kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 ,mgomo wa madaktari nchini Kenya, Tanzania kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, safari za wahamiaji walioko nchini Uingereza kuelekea nchini RwandaTutaangazia pia uchaguzi wa wabunge nchini Togo,usalama wa Burkina Faso , na Ulimweguni  tutazidi kuangazia Mzozo unaondelea baina ya Israel na Hamas .

  • Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC

    20/04/2024 Duration: 20min

    Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.

  • Miaka 30 ya mauaji ya kimbari Rwanda, UN yaondoa jeshi lake DRC na mengineyo duniani

    13/04/2024 Duration: 20min

    Makala yameangazia mambo mengi ikiwemo maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yanaendelea wiki hii, MONUSCO kuanza kuwaondoa wanajeshi wake eneo la mashariki mwa DRC, mgomo wa madaktari nchini Kenya, mwaka mmoja wa mzozo wa Sudani kutimia jumatatu ya aprili 15 na mengineyo duniani. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi

  • Maadhimisho ya miaka 30 mauaji ya kimbari nchini Rwanda, uteuzi wa waziri mkuu mpya DRC

    06/04/2024 Duration: 20min

    Ni makala maalum, kuhusu kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, tunahoji mchakato wa maridhiano umefikia wapi miaka 30 baadaye..... hali iko vipi kwa sasa. na dunia imepata  somo gani? Pia kuhusu mauaji hayo, tutarejelea kauli ya Rais Emanuel Macron iliyoonekana kuwa inalenga kutuliza hisia za waathiriwa.Huko DRC uteuzi wa Judith Tuluka Suminwa, mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu. Mahakama nchini Uganda ilitoa uamuzi wake kuhusu sheria dhidi ya ushoga. Kabla ya kwenda Kenya, Sudani..pamoja na Senegal ambako Bassirou DF aliapishwa kuwa rais mpya, tutakwenda Israeli na maeneo mengine duniani.

  • Diomaye Faye kuapishwa jumanne kama rais wa Senegal, ziara ya rais wa DRC Mauretania

    30/03/2024 Duration: 20min

    Rais mteule wa senegal akutana na rais anayemaliza muhula wake Macky Sall, chama kipya cha aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma chazuwiwa kushiriki uchaguzi wa mwezi mei,kamati ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa, yaitaka Uingereza kuachana na mpango wake wa kuwahamisha wahamiaji kwenda nchini Rwanda, na rais wa DRC Félix Tshisekedi ahitimisha ziara yake huko Mauretania, tutaangazia siasa za Kenya, Tanzania, yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani.

  • Rais Museveni amteua mwanae kuwa mkuu wa majeshi, kifo cha okende kilipangwa

    23/03/2024 Duration: 20min

    Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka

  • Kagame akubali kukutana na Tshisekedi, upinzani Burundi wamfukuza rais wake chamani, Ousmane Sonko aachiwa kule Senegal...

    16/03/2024 Duration: 19min

    Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda. Tutatupia jicho hali ya kibinadamu nchini Sudan, lakini pia siasa za Senegal baada ya kuachiwa kwa Ousmane Sonko, siku chache kabla ya uchaguzi wa Machi 24, kule Nigeria tutaangalia yanayojiri baada ya wanafunzi kutekwa na rais Tinubu kusema hawatatii agizo la watekaji la kutaka kulipwa ili kuwaachia wanafunzi hao.Pia hali kule Haiti baada ya waziri mkuu Ariel Henry kukubali kujiuzulu, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada kutoka Cyprus kuwasili Gaza na pia siasa za Marekani baada ya rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump kushinda uteuzi katika vyama vyao.Niliyeshika usukani ni Jupiter Mayaka kwa niaba ya Ruben Lukumbuka ambaye yuko Pwani ya Kenya anakula upepo wa bahari. Kwa mengi zaidi bonyeza linki usikilize

  • Mashirika ya misaada yatatizika kuhudumia wakimbizi DRC, Ufaransa yahalalisha uaviaji

    09/03/2024 Duration: 20min

    Hali ya usalama kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC baada ya waasi wa M23 kuteka miji kadhaa kama Nyanzale na maeneo jirani, wabunge nchini Uingereza kupinga mpango wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, uchaguzi wa urais kufanyika marchi 24 nchini Senegal, mpya wa 32 wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.

  • Kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, hali ya usalama DRC na mengineyo

    02/03/2024 Duration: 20min

    Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, na kauli za rais Felix Tshisekedi kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na rais mwenza wa Rwanda Paul Kagame, ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Tanzania na pia Kenya, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Arusha, yaliyojiri nchini Rwanda, kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.

  • Rais wa DRC F.Tshisekedi kudumisha amani na jirani zake, mazishi ya mwanariadha Kiptum

    24/02/2024 Duration: 20min

    Makala hii imeangazia kuzorota kwa hali ya usalama pembezoni mwa mji wa Sake DRC,na kauli za rais Felix Tshisekedi mbele ya wanahabari wiki jijini Kinshasa, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Mbeya, mazishi ya mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum, yaliyojiri nchini Rwanda, na pia kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.

  • Mashambulio mjini Sake mashariki ya DRC, hali ya Kenya, kifo cha mpinzani wa Urusi

    17/02/2024 Duration: 20min

    Wiki imejaa matukio ya kutamausha kwanza; wanajeshi wawili wa Afrika kusini waliuawa mashariki mwa DRC, kinara wa upinzani wa nchini Kenya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, maandamano ya wapinzani nchini Tanzania, yaliyojiri Sudani, pia Senegal huko Afrika magharibi, kifo cha mpinzani huko Urusi Alexei Navalyn, shinikizo za kimataifa dhidi ya Israeli ikubali kusitisha vita dhidi ya Hamas,na mengineyo

  • Usalama waendelea kuzorota mashariki DRC,UN na hali ya Sudan

    10/02/2024 Duration: 20min

    Hali ya wasiwasi iliyoshuhudiwa kwenye mji wa Goma, baada ya waasi wa M23 kuonekana kuukaribia mji huo huko mashariki mwa DRC,ziara ya rais wa Poland nchini Kenya na huko Rwanda, kuapishwa kwa rais mpya wa muda nchini Namibia baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hague GeinGhob, yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika magharibi pia uteuzi wa baraza jipya la mawaziri nchini Ufaransa, siasa za Marekani na kwengineko duniani

  • Watatu wafa katika mlipuko wa gas jijini Nairobi Kenya, M23 waendeleza mapigano DRC

    03/02/2024 Duration: 20min

    Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.

  • Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC

    27/01/2024 Duration: 20min

    Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,

  • Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado

    20/01/2024 Duration: 20min

    Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba  kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.

  • Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda

    13/01/2024 Duration: 20min

    Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.

  • Dunia yakaribisha mwaka mpya, mvutano kati ya rais Ruto na idara ya mahakama

    06/01/2024 Duration: 20min

    Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.

  • DRC: Rais Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi kwa muhula wa pili

    31/12/2023 Duration: 20min

    Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni. Tutaangazia pia mashambulio ya ADF kule Uganda lakini pia mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaopigana Sudan ambao haukufanikiwa, hali kule Nigeria kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Plateau, Urusi kufungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso na ulimwenguni tutazidi kuangazia hali ya vita vya Gaza

page 1 from 2