Jua Haki Zako

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 4:09:17
  • More information

Informações:

Synopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodes

  • Kenya: Pesa za majanga haziwafikii waathiriwa

    31/03/2026 Duration: 10min

    Katika makala haya tunaangazia ripoti  kuhusu ufadhili wa majanga na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo kame, iliochapishwa na masharika kadhaa likiwemo lile la Oxfarm. shaba ikilenga taifa la Kenya, Ripoti hii inaonyesha kuwa licha ya maeneo haya kuathirika zaidi na ukame, mafuriko na mabadiliko ya tabianchi, bado fedha nyingi hazifiki moja kwa moja kwa wananchi wanaohitaji msaada huo zaidi. Ripoti hiyo ya Oxafarm inaonyesha kuwa mfumo wa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi nchini Kenya bado una changamoto nyingi, ikiwemo ukosefu wa uwazi, ushirikishwaji mdogo wa jamii, na utegemezi mkubwa wa fedha kutoka nje masharika ya nje

  • Kenya : Haki za wafanyibiashara wa soko la Kigomba

    28/03/2026 Duration: 10min

    Katika makala haya tunaangazia haki za wafanyibiashara katika soko la Gikomba nchini Kenya. Kwa muda wafanyibiashara hao wamekuwa wakizozana na serikali kuhusu kipande cha ardhi cha soko hiyo. Skiza makala haya kufamu mengi zaidi.

  • Kenya : Haki za watoto wa kurandaranda mitaani

    27/03/2026 Duration: 10min

    Kila mtotto ana haki kwa mjibu wa katiba za kila nchi na maazio ya kimataifa. Katika makala haya tunaanhazia haki za watoto wa kurandaranda mitaani. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • EAC : Wanawake wasilia nyuma katika harakati za amani

    09/03/2026 Duration: 10min

    Kila Machi nane dunia, huadimisha siku ya kimataifa ya wanawake, katika makala haya tunaangazia sababu ambazo zimechangia wanawake kuachwa nyuma katika harakati za kutafuta amani. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Haki za wakimbizi wanapokimbilia mataifa ya kigeni

    26/02/2026 Duration: 10min

    Je ni masaibu gani wanayopitia wakimbizi wakati wanapokimbia nchi zao? Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya: Mchakato wa kutoa taarifa za rushwa kwa tume ya EACC

    23/02/2026 Duration: 09min

    Nchini Kenya tume ya kupambana na rushwa EACC imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mali ya umma haiporwi. Ila ni mchakato upi mtu anastahili kufuata kutoa taarifa kwa tume. Benson Wakoli alikiti chini Kipsang Sambae afisa wa EACC, tawi la Nakuru kufahamu mchakato wa kutoa taarifa kwa EACC.

  • Haki ya kuhifadhi taarifa za Siri

    09/02/2026 Duration: 09min

    Je unafahamu kuhusu haki ya taarifa zako za siri kuhifadhiwa? na je unatambua hatua unazostahili kufuata iwapo zitatolewa? .

  • Human Right Watch : Haki zinakandamizwa pembe ya Africa

    09/02/2026 Duration: 09min

    Makala haya yanaangazia ripoti  ya Human Rights Watch iliyochapishwa tarehe 4 Februari 2026, inayozungumzia hali ya kutisha ya haki za binadamu katika eneo la Pembe ya Africa. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa raia wa Sudan, Sudan Kusini na Ethiopia ndio wanaobeba mzigo mkubwa wa vita vya silaha vinavyoendeshwa kwa ukatili, ambapo pande zinazopigana mara nyingi hulenga raia kimakusudi. Human Rights Watch inasema mashambulizi haya dhidi ya raia yamekuwa jambo la kawaida, huku wahusika wakikosa kuwajibishwa. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • Kenya: Hatua za kutafuta haki kwa dhulma za kinadada mtaani Mathare

    27/01/2026 Duration: 09min

    Kwa miaka mingi Beatrice Karole amekuwa akijitolea kuhamasisha jamii kuhusiana na hatua za kuchukua wakati wanapokabiliana na unyanyasaji wa jinsia. Akiwa na shirika la kinamama la Wanawake Mashinani Initiative katika eneo la Mathare Jijini Nairobi, amefanikiwa kuwaokoa jumla ya wanawake na watoto 30 katika mwaka 2025 ambao anajivunia kuwa licha ya kunyanyaswa, walipata haki yao.

  • Kenya: Wakulima wadogowadogo washinda kesi ya Sheria ya Mbegu na Mimea dhidi ya KEPHIS

    25/01/2026 Duration: 21min

    Nchini Kenya, Sheria ya Mbegu na Mimea (The Kenya Seed and Plants Varieties Act), ambayo ilitishia kuwatoza faini na kuwafunga jela wakulima wadogo kwa kugawana mbegu ambazo hazijaidhinishwa, iliamuliwa kuwa kinyume cha katiba. Mahakama ya Kikatiba katika kaunti ya Machakos nchini Kenya ilitoa uamuzi wa kihistoria Novemba 27 2025 kuhusu uhalali wa Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea. George Ajowi amekuwa akifuatilia kesi hii na kuandaa taarifa ifuatayo.

  • EAC : Dhuluma za kijinsia bado ni changamato kote duniani

    10/01/2026 Duration: 10min

    Makala haya yanaangazia namana gani dhuluma za kijinsia zinaweza kabiliwa. skiza kufahamu mengi zaidi.

  • Kenya : Biashara ya ngono miongoni mwa vijana ni donda sugu

    07/01/2026 Duration: 09min

    Juhudi za pamoja zinaendelezwa ili kukomesha biashara haramu ya wototo pwani ya Kenya. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

  • Kenya : Ahadi ya serikali kwa jamii za wachache

    23/12/2025 Duration: 09min

    Kila disemba 18 dunia huadimisha siku ya  Kimataifa ya Jamii za Walio Wachache  siku inayolenga kuzikumbusha serikali na jamii wajibu wa kulinda haki, heshima na ushirikishi wa makundi ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakidai kuachwa nje mipango ya serikali Nchini Kenya, jamii za walio wachache, zikiwemo jamii za wafugaji wanaohamahama, zimekuwa zikidai hazitambuliwi kikamilifu, kukosa huduma za msingi, na kutengwa katika maamuzi muhimu ya kitaifa. Makala haya yanaangazia mipango ya serikali ya Kenya kwa jamii hizo.

  • Mpango wa kidijitali uliokwama unavyowanyima wanafunzi elimu ya kisasa Kenya

    21/12/2025 Duration: 10min

    Mwaka 2016, Serikali ya Kenya ilizindua Mpango wa Mafunzo kwa Njia ya Kidijitali (DLP), ikiahidi kubadilisha elimu ya msingi ya umma kupitia teknolojia. Awamu ya kwanza ikigharimu walipa kodi zaidi ya Shilingi bilioni 30, huku kukiwa na mpango wa kupanua mradi huo kwa makadirio ya Shilingi bilioni 64. Takribani miaka kumi baadaye, mpango huo unazidi kukabiliwa na matatizo makubwa na hatimaye kukwama hivyo kuwanyima wanafunzi wa shule za msingi haki zao za kupata elimu ya kidijitali.Sikiliza

  • Kenya : Haki ya wafanyakazi nje ya nchi

    19/12/2025 Duration: 09min

    Katika Juhudi za raia wa Africa Kutafuta ajira nje ya nchi wengine wamejipata katika njia panda. Lakini ubalozi wa Austria nchini Kenya, unasisitiza taifa hilo ni salama kwa wafanyakazi wa kigeni. Skiza makala haya.

  • EAC : Haki ya matumizi ya mitandao

    02/12/2025 Duration: 09min

    Je unafahamu haki zako wakati unatumia mitandao? na Je unafahamu kwamba haustahili kuvuka kiwango fulani wakati unatumia mitandao? Paul Brain ni mtaalamu  wa matumizi ya mitandao anafanunua masharti ya matumizi ya mitandao.

  • Kenya: Msimamo wa wavuvi wa Lamu kuhusu mbinu za kuvua samaki

    29/11/2025 Duration: 09min

    Kwa muda sasa wavuvi kutoka kaunti ya Lamu, nchini Kenya, wamekuwa wakizozana na serikali kuhusiana na mbinu za kisasa wa uvuvi kutokana na misimo wa serikali kuwataka watumie technolojia katika uvuvi. Mwaka 2016 serikali ya Kenya ilipitisha sheria ya kuwataka wavuvi kutumia mbinu za kisasa kuendesha shughuli za uvuvi lakini hili limeibua changomoto miongoni mwa wavuvu wanaosisitiza kutumia mbInu za kale kuendesha shughuli za uvuvi kutokana na sababu kadhaa. skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

  • Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa

    20/11/2025 Duration: 09min

    Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa.   Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu na kupiga marufuku tendo hilo.   Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya. Katika makala haya  tunaangazia namna tamaduni hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu na kuishi bila unyanyasaji.

  • Matumizi ya hadithi kupigania haki

    17/11/2025 Duration: 09min

    Katika makala haya tunangazia safari ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia hadithi sauti moja, uzoefu, na ujasiri wa mtu kusimulia alichopitia. Tasisi ya  Moth, imekuwa ikitumia hadithi kama si tu kwa mudhadha wa burudunai bali ni daraja linalounganisha ukweli wa mtu mmoja na uelewa wa dunia nzima.  Hadithi nyingi ni za binafsi, lakini hisia zinazozibeba—hofu, matumaini, maumivu au ushindi—ni za ulimwengu mzima. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Mila zanakandamiza wanawake nchini Kenya

    17/11/2025 Duration: 09min

    Mila na tamaduni kutoka jamii mbalimbali nchini Kenya,  zimezidi kukandamiza wanawake kutoridhi mali. Pwani ya Kenya, changamoto hiyo pia imeathiri wanawake wajane skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

page 1 from 2